Responsive image
Responsive image
Posted : April 18, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Responsive image

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amewafukuza kazi zaidi ya majaji 250 kwa kutokuwa na shahada ya sheria na baadhi yao kwa kukabiliwa na tuhuma za rushwa.

Waziri wa sheria wa nchi hiyo Alexis Mwamba ametangaza uamuzi huo wa Rais Joseph Kabila kupitia runinga ambapo amesema Rais Kabila amewafuta kazi majaji hao kwa kutokidhi  vigezo vya kielimu kutekeleza majukumu yao kama majaji.

Hii sio mara ya kwanza kwa serikali ya DRC kuwachukulia hatua maafisa wa juu wa idara ya Mahakama kwani mwaka 2009, Rais Joseph Kabila aliwafuta kazi Majaji 96 baada ya kuwatuhumu kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Hatua hii inakuja ikiwa imesalia miezi 7 kufanyika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment