Responsive image
Responsive image
Posted : April 17, 2018 (7 days ago) By TBC
Responsive image
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Responsive image

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka viongozi wa dini nchini kuanzisha kamati za amani kila mkoa na ngazi ya taifa ili kuwafundisha watu wote umuhimu wa amani kwa ajili ya kufikia maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika mkutano wa kamati ya amani ya mkoa wa Dar es Salaam inayoongozwa na Sheikh wa mkoa huo Alhad Musa Salum, Mzee Mwinyi amesema amani ndiyo kichocheo cha maendeleo, ikizingatiwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt. John Magufuli ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir amesema amani ni jambo muhimu na lizungumzwe kila mahali hasa kwa vijana .

GRACE KINGALAME

APRILI 16, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment