Responsive image
Responsive image
Posted : April 15, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waathrika wa kemikali za sumu wakipatiwa matibabu nchini Syria
Responsive image

Wataalam wa masuala ya kemikali wanatarajiwa kutembelea eneo ambalo inasemekana majeshi ya serikali ya Syria yalitumia kemikali za sumu kuwashambulia raia huko Douma.

Wachunguzi hao wa kimataifa nawararajiwa kutoa majibu kama ni kweli serikali ya Syria ilitumia kemikali za sumu kuwashambulia waasi katia eneo hilo la Douma, ambako waathirika wakubwa wa mashambulio hayo walikuwa ni watoto.

Wachunguzi hao wa kimataifa wanakwenda Douma zikiwa zimepita saa chache tangu nchi ya Marekani na nchi washirika ilipofanya mashambulio dhidi ya serikali ya Syria ikiwa ni sehemu ya kulipiza kisasi baada ya shambulio hilo la sumu.

Marekani inadai imeishambuli Syria ikiwa ni hatua ya kukasirishwa na hatua ya majeshi ya serikali ya nchi hiyo kuwashambulia raia wake wenyewe kwa sumu.

Russia na nchi zinazomuunga mkono rais Bashar Alassad wa Syria zinasema ni jambo la kusikitisha kuona kuwa Marekani imefanya mashambulio hata bila kusubiria matokeo ya uchunguzi utakaofanywa na wachunguzi wa masuala hayo ya kemikali za sumu.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment