Responsive image
Responsive image
Posted : April 14, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Jeneza lililobeba mwili wa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Mandela lilipokuwa likiingizwa uwanja wa Orlando kwa heshima za mwisho
Responsive image

Maelfu ya watu wamejitokeza katika uwanja wa  Orlando mjini Soweto kwa ajili ya kushiriki sherehe za mazishi ya Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela ambae amezikwa leo nchini Afrika Kuisni.

Msemaji wa serikali ya Afrika Kusini Phumla William amesema uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watu 36000 umejaa sana hivyo ilibidi wananchi waombwe kwenda kwenye uwanja wa mchezo wa Raga uliopo karibu na uwanja wa Orlando kufuatilia tukio hilo la kihistoria.

Viongozi mbalimbali wa taifa la afrika kusini pamoja na familia ya marehemu winnie mandela wamemzungumzia winnie wakati wa sherehe hizo.

Akitoa hotuba ya wasifu wa marehemu, Rais wa sasa wa taifa hilo Cyril Ramaphosa amemtaja mwanaharakati huyo kuwa mama, dada, bibi na kiongozi mashuhuri na hadi kufikia hatua ya kuitwa mama wa taifa hilo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment