Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga kupunguza tatizo la msongamano wa mama wajawazito katika hospitali na vituo vya afya kwa kutenga zaidi ya Shilingi Bilioni Mia Moja ambazo zitatolewa kwa wilaya 67 katika kipindi cha mwaka 2018/2019.

Akijibu swali Bungeni Dodoma Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema pamoja na kutoa fedha hizo serikali inaendelea na mpango wa kujenga vituo vya afya kila kata na zahanati kila kijiji ili kuboresha huduma za afya.

Waziri wa Nishati Dkt. Medrad Kalemani amesema mradi wa umeme wa maji katika Mto Malagalasi Mkoani Kigoma ambao ulikuwa utekelezwe mwaka 2008 utaanza kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha baada ya taratibu kukamilika.

Kuhusu tatizo la kukatika katika umeme Jijini Dar es salaam Dkt. Kalemani amesema tatizo hilo linatokana na hitilafu ndogo ndogo na kwamba mikoa ya Lindi na Mtwara hivi karibuni itaunganishwa katika gridi ya taifa, hatua ambayo itapunguza tatizo la kupatikana kwa umeme wa uhakika katika mikoa hiyo.

Kuhusu suala la upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Kigoma na Kagera kupitia mpango wa kusambaza Umeme Vijijini (REA) Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema vijiji 22 vitapatiwa umeme kupitia REA Awamu ya tatu katika mikoa hiyo ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 8.5 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment