Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
Responsive image

Viongozi mbalimbali wamemwelezea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa ni kiongozi aliyeweka misingi imara ya uongozi na kwamba misingi hiyo inapaswa kuenziwa na kurithishwa kwa vizazi vijavyo.

Wakizungumza katika Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini DSM viongozi hao wamesema Mwalimu Nyerere ana kila haja ya kukumbukwa na kuenziwa.

Kongamano hilo limebeba kauli mbiu Kuelekea Uchumi wa Kati, Mchango wa Baba wa Taifa katika Amani, Umoja wa Kitaifa na Uwajibikaji.

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Jijini DSM, Profesa Marc Mwandosya amesema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alikuwa mtu wa watu na mwenye kufuata misingi ya uadilifu.

Mgeni Rasmi katika kongamano hilo Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amemwelezea Baba wa Taifa kuwa alikuwa kiongozi aliyehimiza wananchi wafanye kazi kwa bidii na kukemea tabia ya uchu wa madaraka na kujulimbikizia mali.

Utaratibu wa kuenzi kumbukumbu za viongozi waasisi wa mataifa, kumbukumbu hizo zirisishwe katika vizazi vijayo ili hekima na busara zao ziendelezwe kwa vizazi hivyo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment