Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda
Responsive image

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amesema kupitia zoezi la kusikiliza malalamiko ya akina mama waliotelekezewa watoto tayari familia zaidi ya mia mbili wamekiri kuhudumia watoto wao.

Makonda amesema hayo jijini Dar es salaam wakati wa kuhitimisha siku tano za kuwasikiliza akina mama hao na kusema nia ya Serikali ni kuona mtoto anapata haki yake kwa mujibu wa sheria.

Flora Masue ni Afisa wa ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es salaam ambaye amesema moja ya changamoto iliyopo kwa jamii ni ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusiana na haki za mtoto.

Wengi wa wanawake waliosikilizwa katika zoezi hilo wamempongeza mkuu huyo wa mkoa na kusema zoezi hilo ni fundisho kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.

Zaidi ya wanawake elfu nne wamesikilizwa katika zoezi hilo na watoto zaidi ya mia tano wamesajiliwa kwaajili ya bima ya Afya.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment