Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Responsive image

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema serikali inaendelea kuhakikisha fedha za umma zinazokusanywa kama kodi zinatumika kwa uadilifu kwa ajili ya kuendesha serikali na miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.

Waziri Mpango ametoa kauli hiyo mjini Dodoma akiwa ni miongoni mwa mawaziri waliokutana na waandishi wa habari kwa lengo la kujibu hoja zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali ( CAG).

Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali imejipanga kujibu Hoja za CAG kupitia kwa Mawaziri ili Wananchi waelewe Serikali inachofanya

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo, amesema Wizara yake imechukua hatua dhidi ya Watumishi walioshindwa kutekeleza majukumu yao

IDD MAALIM

12 APRIL 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment