Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo
Responsive image

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la  Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika vyeo mbalimbali.

Akisoma taarifa ya uteuzi huo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, amesema Rais Magufuli amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Massao kuwa Luteni Jenerali.

Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli -TMA na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.

Rais Magufuli amempandisha cheo Brigedia Jenerali Henry Kamunde kuwa Meja Jenerali.  Hali kadhalika Rais Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali na Afisa mmoja kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.

Waliopandishwa vyeo hivyo ni Mullugu, Mwaseba, Mwamy, Kapinda, Katenga, Kiwenge, Mgambo, Alphonce, Mutta, Chakila, Mhagama, Kisiri, Msolla na Mzee. Wengine ni Ndiege, Mhona, Ng’umbi, Mnkande, Sibuti, Mumanga, Ismail, Mkeremy, Mhidze, Machanga, Gwaya, Simuli na Gaguti.

 Rais Magufuli pia amempandisha cheo Luteni Kanali Bernard Mlunga kuwa Kanali na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais.

Kanali Mlunga ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mbaraka Mkeremy ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment