Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen
Responsive image

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen ametoa wiki moja kwa Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  kwa kushirikiana  na jeshi  la polisi wilayani Kilosa  kumtafuta mkandarasi SIHA ENTERPRISES aliyeshindwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara za Kilosa Uhindini kwa wakati licha ya kulipwa fedha za ujenzi.

Dkt Kebwe ametoa agizo hilo baada ya kutembelea barabara hizo ambazo kwa sasa zipo chini ya wakala wa barabara Mijini na Vijijini TARURA na kusisitiza  serikali mkoani humo  haitawavumilia wakandarasi  wanaoshindwa kukamilisha miradi kwa wakati .

Naye mkuu wa wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amemtaka Mkurugenzi Mtendaji  kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya watendaji wa serikali waliopewa dhamana ya kuusimamia mradi huo na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

MONICA LIAMPAWE

APRILI 12, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment