Responsive image
Responsive image
Posted : April 11, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli
Responsive image

Rais John Magufuli amezindua Taasisi ya Jakaya Kikwete na kusema kuwa serikali iko tayari kushirikiana na taasisi hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es salaam Rais Magufuli ameyataja maeneo manne ambayo taasisi hiyo imechagua kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kusimamia afya ya mama na mtoto, maendeleo ya vijana, kilimo pamoja na utawala bora.

Amesema serikali haitafumbia macho taasisi yoyote ya kiraia itakayotaka kuvuruga amani na maadili ya Kitanzania.

Pia amezitaka taasisi na wadau mbalimbali kuiunga mkono taasisi ya Jakaya Kikwete katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema lengo kuu la taasisi hiyo  kuchangia katika kupunguza umasikini na kuimarisha usalama wa chakula ili kuongeza nguvu katika maendeleo.Kaulimbiu ya Taasisi hiyo ni Kuboresha maisha ya watu kwa ushirikiano

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Prof. Isaya Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Jairo unaanza leo.

Profesa Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi –ITA, na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika.

AGNES MBAPU

APRILI 11, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment