Responsive image
Responsive image
Posted : April 11, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Dare es salaam Paul Makonda
Responsive image

Mkuu wa mkoa wa Dare es salaam Paul Makonda amesema ofisi yake itatoa bima ya afya bure kwa watoto wote waliofikishwa katika ofisi hiyo na kudhihirika kuwa wametelekezwa.

Makonda amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na  wananchi waliokwenda kupata msaada kwa ajili ya watoto waliotelekezwa.

Siku ya tatu tangu Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa DSM ianze kusikiliza madai ya wanawake waliotelekezwa pamoja na watoto wao, wakinamama wameendelea kufika katika ofisi hizo kwa wingi.

Makonda amesema watafanya vipimo vya vinasaba (DNA) na atakayebainika kumtelekeza mtoto wake atalazimika kulipa gharama za malezi ya mtoto husika.

Wazazi wa watoto waliotelekezwa wameshukuru kwa hatua ya watoto wao kupatiwa bima ya afya.

Tangu kuanza kwa zoezi hilo zaidi ya watu 800 wamesikilizwa.

 

ZAITUN KHAMIS

APRILI 11, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment