Responsive image
Responsive image
Posted : April 11, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Picha ya kitanzi (kwa hisani ya mtandao)
Responsive image

Mtu mmoja mkazi wa Manispa ya Bukoba mkoani Kagera amekufa kwa kujinyonga baada ya kupima afya yake na majibu kuonesha ameathirika na virusi vya ukimwi .

Katika ujumbe aliouacha, Seridion Sylvester amesema ameamua kuchukua maamuzi hayo baada ya mkewe kukataa kuishi naye baada ya kumfahamisha majibu ya vipimo vyake.

Mwenyekiti wa mtaa Victor Nshange amesema marehemu pamoja na mkewe Sarafina Anorld walikwenda kupima afya zao na matokeo yakawa si mazuri kwa mume.

Mke wa marehemu, Sarafina, amesema mara baada ya kupatiwa majibu hayo mumewe alimwambia arudi nyumbani kwao pamoja na watoto.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera Charles Mafwimbo amewataka wananchi kuendelea kupima afya zao na kuwa na utayari wa kupokea majibu  sambamba na kufuata ushauri wa kitaalam.

CHARLES MWEBEA

APRILI 11, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment