Responsive image
Responsive image
Posted : April 11, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mshambuliaji nguli wa Atletico Madrid Fernando Torres
Responsive image

Mshambuliaji nguli wa Atletico Madrid, Fernando Torres ataondoka kwenye timu hiyo mwisho mwa msimu huu ingawa hajasema ataenda kucheza soka wapi.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea amesema ameamua kundoka kwenye timu hiyo baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Diego Simione.

Torres maarufu kama El Nino amesema huu utauwa msimu wake wa mwisho kwa na timu hiyo kwa sababu anapata muda muchache mno wa kucheza na yeye anataka apate nafasi ya kucheza mara nyingi awezavyo.

Mshambuliaji huyo alijiunga kwa mara ya pili na timu hiyo iliyomlea mwaka 2014 baada ya kucheza kwenye timu za Liverpool, Chelsea na AC Millan na ameifungia magoli 126 katika awamu mbili za kuichezea. Torres pia alikuwemo kwenye kikosi cha Chelsea kilichotwaa taji la ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2012.

Timu hiyo imesema itamuandalia sherehe maalum ya kumuaga kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi ya Hispania dhidi ya Eibar hapo Mei 20 ya mwaka huu na inafanya hivyo kwasababu huyo ni mchezaji mwenye heshima kubwa kwenye timu yao.

Mwenyewe Torres amemaliza kwa kusema alipanga kustafu kucheza soka akiwa na timu hiyo lakini inabidi aondoke tu na kukiri kuwa hatostafu kucheza soka kwasasa bado atacheza soka kwa miaka miwili, mitatu au mitano ijayo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment