Responsive image
Responsive image
Posted : April 08, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mmoja wa raia wa Syria aliyekuwa mhanga wa shambulio la kemikali lililofanyika nchini humo
Responsive image

Watu wapatao 70 wamekufa katika shambulio linalodaiwa kuwa ni la kemikali katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Douma uliopo mashariki mwa Ghouta nchini Syria.

Vikosi vya uokoaji vya kujitolea vimetuma picha kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha miili ya watu waliokuwa wamekufa na kusema idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Lakini serikali ya Syria imeziita tuhuma hizo za shambulio la kemikali kuwa ni uongo mtupu.

Wakati huo huo wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa taarifa kuwa idadi ya vifo kutokana na shambulio hilo inaweza kuongezeka.

Taarifa hiyo pia imesema Russia ambayo imekuwa inaunga mkono serikali ya Syria inahusika na shambulio hilo.

(CHANZO BBC)

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment