Responsive image
Responsive image
Posted : April 01, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo
Responsive image

Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi, Alinikisa Cheyo, amewataka watanzania kuacha kulalamika lalamika na badala yake kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo wao wenyewe na kuliletea maendeleo taifa.

Alikuwa akihutubia wakati wa ibada ya pasaka iliyofanyika kitaifa katika kanisa la Moravian Tanzania ushirika wa Mbeya mjini, mkoani Mbeya, ibada ambayo ilirushwa mubashara na vyombo vya Shirika la Utangazaji Tanzania vya TBC1, TBC2 na TBC Taifa.

Askofu Cheyo amesema kaulimbiu ya Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli ya 'Hapa Kazi tu' inapaswa kuthaminiwa kwani ndio msingi wa maendeleo.

Akizungumzia chaguzi zinazokuja za Serikali za Mitaa (2019) na Uchaguzi Mkuu (2020) Askofu Cheyo amesema inapaswa kila mtanzania kuhakikisha kuwa amani inakuwepo kwa kulinda umoja wa kitaifa badala ya kusimamia migawanyiko kivyama au kiitikadi.

"Wanasiasa inapaswa wajue kwamba sio kila mtanzania ni mwanachama wa chama fulani" alisema na kuongeza kuwa watanzania walioko kwenye vyama hawafiki milioni 10 katika nchi yenye watu karibu milioni 50, hivyo wanasiasa wajue kuwa wananchi  walio wengi bila ushabiki wa vyama ni watanzania na wanastahili kuishi kwenye nchi yao kwa amani.

ASTERIUS BANZI

APRILI 1, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment