Responsive image
Responsive image
Posted : March 30, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Bango linaloelezea umuhimu wa chandarua kwa kujikinga na malaria
Responsive image

Wananchi Visiwani Zanzibar wametakiwa kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria hasa katika kipindi hiki cha mvua ambapo kunakuwa na mazalia mengi ya mbu wanaoambukiza ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja  meneja wa  mradi wa  kudhibiti malaria wa wizara ya afya  Zanzibar Abdalla Ali Said amesema kipindi cha mwezi juni,julai na agosti kuna mambukizi ya ugonjwa huo yanayotokana na sababu mbalimbali ikiwemo uwepo wa mazalia mengi ya mbu .Zanzibar,  Kisiwa kilichofanikiwa kudhibiti  ungojwa wa malaria kwa kiasi kikubwa.

Takwimu kutoka Wizara ya Afya Kitengo cha Kudhibiti Ungonjwa huo zinaeleza kuwa miaka kumi iliyopita asilimia 32 ya vifo vilivyotokea kwa mwaka vilisababiswa na ugonjwa huo tofauti na mwaka 2015, 2016 na 2017.

Shirika la afya duniani WHO limeeleza kuwa ili kudhitibi ugonjwa huo ni lazima matumizi ya vyandarua, upigaji wa dawa majumbani na elimu ya afya itolewa kwa jamii kwa asilimia isiyopungua 85 ambapo Zanzibar wameunga mkono kauli hiyo kwa kuzindua mradi wa matumizi bora ya vyandarua.

Baadhi ya wananchi wamesema jitihada za kudhibiti ugonjwa huo zimeleta manufaa makubwa.

Wamesema katika kipindi hiki cha mvua jamii haina budi kuhakikisha mazingira yao yanakuwa  katika hali ya usafi kwa kuondoa mazalia ya mbu.

SWAUMU MAVURA

30 MACHI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment