Responsive image
Responsive image
Posted : March 30, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya vifaa vya redio za FM
Responsive image

Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imevifungia zaidi ya vituo 20 vya redio vya FM kwa tuhuma za kukiuka taratibu za kitaaluma.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ya Mawasiliano Godfrey Mutabazi amesema vituo hivyo vilivyofungiwa vinashutumiwa kwa kutangaza uganga wa kienyeji na kuwatapeli wananchi. Mutabazi ameshutumu redio hizo kutumiwa na waganga wa kienyeji kuwatapeli wananchi na kuvunja sheria ya uchawi.

Amesema redio hizo zimekuwa zikiwapa vipindi waganga hao wa kienyeji kutangaza uganga wao, huku wakiwaambia wananchi kutuma fedha kupitia njia ya simu za mikononi.

Miaka ya nyuma Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewahi kutishia kuvifungia vituo vya redio ambapo mara kadhaa polisi wamekuwa wakivamia baadhi ya vituo vya habari.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment