Responsive image
Responsive image
Posted : March 24, 2018 (4 weeks ago) By TBC
Responsive image
Askari nchini Ufaransa wakiwa nje ya eneo la duka kubwa ambalo lilivamia na mshambuliaji Ijumaa
Responsive image

Askari ambaye alijitolea kushikiliwa mateka badala ya mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa mateka walioshikiliwa na mshambuliaji ndani ya duka kubwa kusini mashariki mwa mji wa Trebes(TREB) nchini Ufaransa,  amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata. 

Mwendesha mashtaka wa Paris, Francois Molins amesema askari huyo, Luteni Kanali Arnaud Beltrame (44), alihatarisha maisha yake kwa kuingia kwenye duka walikokuwa wanashikiliwa mateka ili kuokoa watu hao.

Kijana mwenye silaha aliyetambulika kama Redouane Lakdim (25) alivamia duka moja kubwa na kuwapiga risasi wafanyakazi wawili wa duka hilo, kisha kuwashikilia mateka watu wengine waliokuwemo humo.

Taarifa zimesema polisi walifanikiwa kuwatoa nje baadhi ya mateka wakiwa salama, lakini walishindwa kumshambulia mtekaji huyo aliyekuwa amemtanguliza mbele mwanamke mmoja aliyemtumia kama kinga, ndipo Beltrame alipojitolea kubadilishana na mwanamke huyo, huku akiwa ameacha simu yake mezani 'line' ikiwa wazi kuwawezesha askari wenzake walioko nje kuweza kufuatilia yanayotokea ndani.

Polisi waliweza kusikia milio ya risasi na wakaamua kikosi maalum cha mashambulizi kivamie ndani ya duka hilo, hatua iliyowawesha kumuua mshambuliaji huyo, lakini pia kumuacha Beltrame akiwa amejeruhiwa vibaya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemuelezea askari huyo kuwa ni shujaa aliyekuwa tayari kuweka maisha yake hatarini kwa ajili ya kuokoa wengine na ni  na mtu mwenye ujasiri wa pekee.

Inasemekana Lakdim ni mfuasi wa kikundi cha wapiganaji wa Islamic State na kuwa alidai kuachiwa huru kwa Salah Abdeslam ambae ni mtuhumiwa wa shambulio la kigaidi lililotokea mjini Paris nchini Ufaransa mwezi novemba mwaka 2015 shambulio ambalo lilisababisha vifo vya watu 130.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment