Responsive image
Responsive image
Posted : March 22, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amemwakilisha Rais John Magufuli kwenye kikao cha Afrika, Kigali Rwanda
Responsive image

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepongeza makubaliano yaliyofikiwa na nchi za Afrika ya kulifanya bara hilo kuwa eneo huru kibiashara.

Majaliwa ameyasema hayo Jijini Kigali, Rwanda baada ya kumaliza kusaini mkataba wa nchi za Afrika ambapo amemwakilisha Rais John Magufuli

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Kigali ,Waziri Mkuu Majaliwa amesema Tanzania imeajiandaa vya kutosha kutekeleza mkataba huo na kwamba itahakikisha mkataba huo unatelekezwa bila kuathiri uzalishaji na sera za ndani.

Mikataba iliyosaioniwa na mataifa hayo 50 ya Bara la Afrika ni pamoja na mkataba wa kulifanya Bara la Afrika kuwa eneo huru la biashara, Itifaki ya kisheria ya utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwamo uhuru wa makazi, haki ya kuishi na kufanya kazi popote bila vikwazo wala vizuizi vyoyote.

Awali akihutubia katika ufunguzi wa sherehe hizo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), ameyataja maeneo makuu ambayo mkataba huo umeangazia kuwa ni pamoja na eneo huru la biashara ya anga, miundombinu ya reli na barabara ambayo itaziunganisha nchi za Afrika kuwasiliana kwa urahisi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment