Responsive image
Responsive image
Posted : March 14, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli akizindua ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Dodoma
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli ameweka jiwe la msingi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma na kusema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi ikiwemo kuongeza kasi ya maendeleo na kutengeneza ajira elfu 30 wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Rais Magufuli ametoa wito kwa mkandarasi wa ujenzi wa reli hiyo itakayogharimu Shilingi zipatazo Trilioni 15 kukamilisha mradi kwa wakati.

Aidha kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika utakaosaidia kufikia azima ya uchumi wa kati na nchi ya viwanda Rais Magufuli amesema mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge utaongeza upatikanaji wa umeme wa uhakikika.

Amesema serikali imeazimia kutengeneza ajira kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, barabara, madaraja, umeme vijijini na ukarabari wa viwanja vya ndege, ujenzi wa meli kubwa katika Ziwa Victoria na miradi mingine.

Kuhusu masuala ya kodi Rais Magufuli ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato pamoja na kuwadhibiti watendaji ambao sio waaminifu.

Amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama na watanzania kwa ujumla kwa kudumisha amani na usalama wa nchi kwani vitu hivyo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa ni mmoja wa wageni katika uzinduzi wa reli hiyo ya kisasa ambapo amewataka watanzania kutumia fursa ya ujenzi wa reli hiyo kujiinua kiuchum.

Naye Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amesema tayari mkandarasi amewezeshwa ili asikwame kifedha.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amesema ujenzi wa reli hiyo utasaidia uwekezaji katika mkoa wa Dodoma katika sekta za uchumi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini Masanja Kadogosa amesema bado changamoto kubwa ni kuwaondoa watu waliojimilikisha maeneo ya reli.

Ujenzi wa reli ya kisasa ya kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma una jumla ya kilomita 426  na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36 yaani ifikapo Desemba mwaka 2020.

DOREEN MLAY

MACHI 143, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment