Responsive image
Responsive image
Posted : March 13, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Wanafunzi wa shule ya msingi Msambiazi huko Korogwe wakiwa madarasani
Responsive image

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msambiazi katika Halmashauri ya Mji wa Korogwe mkoani Tanga wako kwenye hatari ya  kuangukiwa na vyumba vya  madarasa kutokana na shule hiyo kujengwa na matofali ya udongo pekee miaka mingi iliyopita.

Darasa la tatu na la nne ndio linalokabiliwa na uchakavu wa kiwango cha juu na kuhatarisha usalama wa wanafunzi katika shule hiyo. 

Akiwa katika ziara kutembelea miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi ,Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mji Merry Chatanda ameitembelea shule hiyo na kujionea hali ya madarasa yanayohatarisha maisha.

Inatazamiwa kuwa vyumba vitatu vya madarasa vinavyojengwa kwa sasa  na serikali kwa ushirikiano na nguvu za wananchi katika shule hiyo yenye wanafunzi 728 vitakapokamilika vitasaidia kumaliza tatizo.

BERTHA MWAMBELA

13MACHI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment