Responsive image
Responsive image
Posted : March 13, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa
Responsive image

Mkoa wa Mtwara umeanza kuhakiki wakulima wa Korosho ambao wanadai malipo yao ya msimu wa mwaka 2016/2017 na mwaka 2017/2018 ili waanze kulipwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema idadi kubwa ya wakulima wanaodai fedha hizo ni kutoka wilaya ya Masasi ambapo wanadai Shilingi Bilioni 1.5.

Kutokana na wakulima wengi wa wilaya za Tandahimba, Newala, Masasi na Mji wa Nanyamba kuendelea kudai malipo ya mauzo ya korosho zao kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na mwaka 2017/2018 Byakanwa amesema wameanza kuhakiki idadi ya wakulima wanaodai ili waweze kulipwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Mtwara, Byakanwa amesema wakulima wa Wilaya ya Masasi ndio wanadai kiasi kikubwa cha fedha kutokana na baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi wa Ushirika kudaiwa kutokuwa waaminifu.

Amesema kiongozi yoyote atakayebainika kujihusisha na ubadhirifu wa fedha za mkulima wa korosho atachukuliwa hatua.

Aidha amesema malipo ambayo yamechelewa yametokana na wakulima wenyewe kushindwa kufungua akaunti hivyo amewataka wakulima kuhakikisha wanafungua akaunti kabla ya msimu kuanza

MARTINA NGULUMBI

13 MACHI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment