Responsive image
Responsive image
Posted : March 13, 2018 (2 months ago) By tbc
Responsive image
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Responsive image

Serikali imewasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa na ukomo wa bajeti kwa mwaka 2018/2019 ambapo zaidi ya Shilingi trilioni 32 zitatumika katika mwaka ujao wa fedha ikiwa na ongezeko la Shilingi Milioni 764 kutoka bajeti ya mwaka 2017/2018.

Akiwasilisha mapendekezo hayo Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango ameeleza vipaumbele katika mapendekezo hayo kuwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es salaam hadi Dodoma, ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa maji Mto Rufiji na ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Tanga hadi Hoima Nchini Uganda.

Dkt. Mpango amewasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa Taifa na kiwango cha  ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2018/19 ikiwa ni mapendekezo ya tatu ya bajeti ya Serikali ya Awamu ya Tano. Baadhi ya wabunge wameipongeza serikali huku wakitoa mapendekezo yao ili kuboresha mapendekezo ya serikali.

SHABANI KWAKA

13 MACHI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment