Responsive image
Responsive image
Posted : March 13, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Washiriki wa mkutano mkuu wa 11 wa vyombo vya utangazaji vya Afrika unaofanyika Kigali, Rwanda
Responsive image

Vyombo vya utangazaji barani Afrika vimeshauriwa kutumia maendeleo ya utangazaji kwa njia ya kidijitali kutangaza habari zinazohusu maendeleo na mafanikio yaliyopatikana katika bara hilo, badala ya kuachia vyombo vya magharibi kupotosha taarifa za wananchi wa Afrika.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Rwanda, Louise Mushikiwabo wakati akifungua mkutano mkuu wa 11 wa vyombo vya utangazaji vya Afrika unaofanyika mjini Kigali  nchini Rwanda

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayub Rioba amesema vyombo vya utangazaji kutoka Afrika vinapaswa kutumia mkutano huo kwa kutatua changamoto zilizokuwepo na kutoa kipaumbele katika kuandaa na kutangaza vipindi vyenye maudhui ya kiafrika

Mkutano Mkuu wa 11 wa vyombo vya utangazaji vya Afrika umepanga kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu maendeleo na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utangazaji wa mfumo wa kidijitali na kuona namna bora ya kukabiliana nazo.

GABRIEL ZAKARIA

13 MACHI 2018 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment