Responsive image
Responsive image
Posted : March 13, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Edna Lema
Responsive image

Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars, Edna Lema amesema ubora wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania bara umeongezeka msimu huu kutokana na uzoefu waliopata kwa asilimia kubwa wachezaji wa ligi hiyo, baada ya kuwa washiriki kwa msimu wa pili sasa.

Akizungumza na TBC, Lema amesema kutokana na kuongezeka kwa ubora huo, baadhi ya wachezaji wamechaguliwa kuunda kikosi cha timu ya Taifa kufuatia uwezo mzuri waliouonyesha kwenye ligi hiyo huku akiwashukuru wadau wa michezo kwa kuiunga mkono ligi hiyo ya wanawake.

Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania bara, ipo kwenye hatua ya nane bora ambapo imesimama kwa sasa kupisha kambi ya timu ya Taifa ya wanawake inayojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za michuano ya mataifa ya Afrika kwa wanawake dhidi ya timu ya Taifa ya wanawake ya Zambia, mchezo utakaochezwa kati ya Aprili 2 na Aprili 10 mwaka huu.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment