Responsive image
Responsive image
Posted : March 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi
Responsive image

Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais Dkt. John magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza rasmi leo Jumatatu jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo kamati iliyoundwa na Rais Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wake Mukesh Bhavnani.

Mazungumzo hayo yana lengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili na kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini.

Kampuni ya Bharti Airtel iliomba kufanyika kwa mazungumzo hayo baada ya kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Dkt. Magufuli.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment