Responsive image
Responsive image
Posted : March 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Naibu waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndungulile
Responsive image

Naibu waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndungulile amesema ugonjwa wa shinikizo la macho umeendelea kuwa tatizo kwa baadhi ya  wananchi kutokana na kukosa elimu sahihi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Dkt Ndungulile  amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu maadhimisho ya wiki ya shinikizo la macho ambayo huadhimishwa kuanzia tarehe Mosi  hadi 17 Machi kila mwaka.

Pia Naibu waziri huyo amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima macho walau mara moja kwa mwaka ili kuzuia ulemavu wa macho unaoweza kusababishwa na ugonjwa huo.

Amesema  elimu pamoja huduma za vipimo vya macho  zinapatikana katika hospitali na vituo vyote vya afya nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.

Kauli mbiu ya wiki ya shinikizo la macho ni 'Okoa Uoni Wa Macho Yako, Nenda Kapime Iwapo Una Shinikizo la Macho'.

ZAITUNE KHAMIS

12 MACHI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment