Responsive image
Responsive image
Posted : March 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza
Responsive image

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ametangazwa rasmi kuwa kiongozi wa kudumu wa chama tawala cha CNDD/FDD.

Maamuzi hayo yamefanyika baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Rais Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.

Taifa la Burundi pia linakusudia kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Chama tawala kimechukua uamuzi wa kumuongezea hadhi na kumpa cheo cha juu Rais Nkurunziza na hivyo kumtangaza kuwa ni kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.

CHANZO BBC

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment