Responsive image
Responsive image
Posted : March 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya wakazi wa Dodoma wakipatiwa stadi za kuwaimarisha kimaisha
Responsive image

Wakazi  zaidi ya elfu moja kutoka vijiji vitano vilivyo kwenye wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma vilivyopisha mradi wa upanuzi wa Ikulu wameshukuru wakala wa majengo Tanzania TBA kwa kuwapatia stadi mbalimbali kupitia VETA.

Wakazi hao wamepatiwa stadi mbalimbali ikiwamo ufundi, ulinzi, upishi na mazingira na kuwapatia ajira katika mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa sera ya TBA ya kuwezesha wakazi walio kwenye eneo linalotekelezwa miradi.

Kwa upande wao viongozi wa maeneo yalionufaika na mpango huo wamesema utaratibu uliofanywa na wakala wa majengo nchini umekuwa msaada wa wananchi walio kwenye eneo hilo.

Mpango huo unaoratibiwa na wakala wa majengo nchini TBA umenufaisha wananchi wa vijiji vya Msanga, Buigiri, Chahwa, Chamwino Ikulu na Vikonji.

ELISHA ELIA

MACHI 12, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment