Responsive image
Responsive image
Posted : March 12, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabudai
Responsive image

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabudai ameshauri kuanzishwa kwa mashindano ya mbio mbalimbali ili kukuza vipaji vya watoto na kuwajengea uwezo wakiwa wadogo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Marathoni za Watoto wa Shule za Msingi na Sekondari zilizoandaliwa na kituo cha michezo cha Shule ya Mtakatifu  Patrick mkoani Arusha,  Gidabudai amesema kukuza vipaji kwa watoto ni njia pekee ya kukuza na kuendeleza michezo hapa nchini na kuwa na wanamichezo wengi nyota wanaotamba kimataifa.

Gidabudai pia amepongeza juhudi za shule hiyo katika kukuza michezo na kutoa wito kwa shule nyingine kuiga.

Michezo mbalimbali imeshindaniwa katika mashindano hayo ambapo watoto wa umri wa miaka saba na kumi na tatu na washindi wamepewa zawadi ya medali za Dhahabu kwa washindi wa kwanza, Fedha kwa washindi wa pili na Shaba kwa washindi wa tatu.

ENOCK BWIGANE

MACHI 13, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment