Responsive image
Responsive image
Posted : March 10, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Rais John Magufuli
Responsive image

Rais John Magufuli ameagiza wananchi waliovamia eneo la Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Mwanva kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wasiondolewe katika eneo hilo kwa kuwa Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na ufundi imeshindwa kuliendeleza kwa muda mrefu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mjini Kahama, Rais Magufuli amesema wananchi hawana kosa kuvamia eneo hilo, lenye zaidi ya hekari mia tatu ambalo limeshindwa kuendelezwa, huku wananchi wakikabiliwa na changamoto ya maeneo kwa ajili ya ujenzi wa makazi.

Alipozungumza na wananchi Rais Magufuli ikamlazimu kwanza kutoa kauli ya serikali juu ya mgogoro wa eneo la Chuo hicho na baadae akapokea kero za wananchi zikiwemo za wachimbaji wadogo. Katika kuwasaidia wachimbaji wadogo ilielezwa kuwa serikali imeshatenga maeneo kwajili yao.

GREYSON KAKURU

10 MACHI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment