Responsive image
Responsive image
Posted : March 10, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu
Responsive image

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoani humo kumkamata na kumfikisha ofisini kwake mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya MECCO ili aeleze sababu za kushindwa kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Bukoba.

Meja Jenerali Mstaafu Kijuu ametoa agizo hilo baada ya Meya wa Manispaa hiyo Chief Kalumuna kumlalamikia mkandarasi huyo kwa kushindwa kusaini mkataba na kuanza  ujenzi wa barabara za manispaa hiyo baada ya kushinda zabuni.

Kalumuna alitoa malalamiko yake kuhusiana na mkandarasi Kampuni ya MECCO iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa barabara kadhaa za manispaa.

Barabara hizo za Manispaa ya Bukoba zinajengwa kwa ufadhili wa Shilingi Bilioni sita kutoka Benki ya Dunia.

CHARLES MWEBEYA

10 MACHI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment