Responsive image
Responsive image
Posted : March 09, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Dkt. John Pombe Magufuli
Responsive image

Rais John Magufuli amesema hatatoa fedha ya wananchi kwa benki yeyote itakayoshindwa kusimama yenyewe.

Magufuli ameyasema hayo alipokua akifungua Tawi la CRDB Chato Mkoani Geita na kusema kuwa benki ambazo zinasuasua ziungane na benki imara ili ziweze kupata faifa.

Awali Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani amewataka wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kuwekeza nchini huku Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel akisema wawekezaji waende kuwekeza Chato kwani kuna fursa nyingi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji amesema huduma za fedha jumuishi zimeongezeka nchini pamoja na Tanzania kuwa ya sita duniani katika huduma za fedha jumuishi.

Benki ya CRDB ina matawi zaidi ya 250 nchini. 

DOREEN MLAY

09 MACHI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment