Responsive image
Responsive image
Posted : March 09, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Rais Kim Jong – Un wa Korea Kaskazini (kushoto) anatarajiwa kukutana na Donald Trump wa Marekani
Responsive image

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un na Rais Donald Trump wa Marekani wanatarajia kukutana mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Taarifa za kukutana kwa viongozi wawili hao zimetolewa na ujumbe wa maofisa wa Korea Kusini baada ya mazungumzo na Rais Trump nchini Marekani.

Maofisa hao wa Korea Kusini walipeleka ujumbe kwa Trump kutoka kwa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong – Un wakisema Rais huyo yuko tayari kuacha kutengeneza silaha za nyuklia.

Taarifa hiyo imekuja siku kadhaa baada ya ujumbe wa Korea Kusini kukutana na Kim mjini Pyongyang.

Katika hatua nyingine Rais Trump ametia saini ushuru wa forodha kwa bidhaa ya chuma na alumini.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment