Responsive image
Responsive image
Posted : March 09, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Kenyatta akiwa na kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga
Responsive image

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchini humo -NASA Raila Odinga wamewataka raia wa Kenya kumaliza tofauti zao ili kulipeleka taifa lao mbele.

Katika mkutano wao wa kwanza tangu uchaguzi, viongozi hao wawili wamesisitiza haja ya kuunganisha nchi yao ambayo hivi karibuni imegubikwa na hofu ya kuvunjika kwa amani kutokana na utofauti wa kikabila, kidini na itikadi za kisiasa.

Wakizungumza nje ya Ikulu ya Harambee baada ya kumaliza mazungumzo yao ndani, Rais Kenyatta amesema Kenya ni kubwa kuliko mtu yeyote na kwamba ili taifa liwe na umoja viongozi wanapaswa kuwa pamoja na kujadili matatizo yanayokabili Taifa.

Viongozi hao wawili wamewataka wakenya kuunga mkono hati ambayo pamoja na mambo mengine, itashughulika na mgawanyiko kwa lengo la kujenga taifa imara ambalo halitamuacha mtu nyuma. 

Kukutana huko kumekuja saa chache kuelekea ziara ya siku nne ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson nchini humo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Afrika.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment