Responsive image
Responsive image
Posted : March 08, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya wanawake wafanyakazi wa TBC wakiwa wamebeba bango lenye kauli mbiu ya siku ya wanawake 2018
Responsive image

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ametoa wito kwa mashirika ya umma, sekta binafsi na asasi za kiraia kushirikiana na serikali kuwawezesha wanawake.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mama Magufuli amesema ni vema mashirika hayo yakawasaidia wanawake kupata mitaji na kuwatafutia masoko.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda ametoa wito kwa wanawake waliotelekezwa na kuachwa na watoto kwenda ofisini kwake kuanzia Aprili 9 mwaka huu.

Katika maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam wanawake wamekutana na kusisitiza umuhimu wa elimu na matumizi sahihi ya rasilimali kwa manufaa ya wanawake

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni Kuelekea Uchumi wa Viwanda Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa wanawake vijijini.

DOREEN MLAY

MACHI 08, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment