Responsive image
Responsive image
Posted : March 06, 2018 (2 months ago) By TBC
Responsive image
Kocha Mkuu wa timu ya Simba Pierre Lechantre
Responsive image

Timu ya Simba imetamba kufanya vyema kwenye mchezo wake wa kwanza mzunguko wa kwanza  wa Kombe la Shirikisho  barani Afrika dhidi ya timu ya Al Masry ya Misri kwenye mchezo utaochezwa kesho kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Kocha Mkuu wa timu ya Simba Pierre Lechantre amesema wapo tayari kuwavaa Wamisri hao huku lengo likiwa ni kupata mabao mengi kwenye mchezo wa nyumbani ili kurahisha kazi kwenye mchezo wa marudiano kauli inayoungwa mkono na nahodha wa timu hiyo  John Bocco ambaye pia amewasisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwaunga mkono.

Endapo Simba itafanikiwa kupita katika hatua hii itasonga mbele katika hatua ya 16 ambapo itacheza mchezo mwingine wa mtoano ili kuingia nane bora ambapo kama itafanikiwa kuingia hatua hiyo itajinyakulia kitita cha Dola za Marekani 275,000 i ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 600 za Tanzania, kama bonasi ya kupenya hatua hiyo.

OSCAR URASSA

MACHI 06, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment