Responsive image
Responsive image
Posted : March 05, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Marehemu Davide Astori aliyekuwa nahodha wa klabu ya Fiorentina ya Italia
Responsive image

Wakazi wa mji wa Florence pamoja na ulimwengu wa mpira wa miguu wanaendelea kuomboleza kifo cha ghafla cha nahodha wa timu ya Fiorentina ya Italia, Davide Astori aliyefariki dunia hotelini kwa kile kilichoelezwa kuwa aliugua ghafla akiwa usingizini.

Taarifa za kifo cha Astori aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 31 zimeacha simanzi kubwa kwa marafiki, familia, klabu yake na taifa la Italia kwa ujumla huku waziri mkuu wa zamani wa Italia ambaye pia amewahi kuwa meya wa mji wa Florence na kiongozi wa chama cha Partito Democratico ambaye ni shabiki  wa kutupwa wa Fiorentina, Matteo Renzi akisema bado haamini kama Astori ameondoka  na kwake ni taarifa ngumu mno kuzisikia.

Imeelezwa kuwa mara nyingi wakati kikosi cha Fiorentina kilipokuwa kikiwasili sehemu yoyote hususani wanaposafiri nahodha  huyo alikuwa wa kwanza kuwahi kupata kifungua kinywa katika hoteli yoyote ambayo timu yake hufikia na jana nahodha huyo hakuonekana kwenye mgawaha uliopo kwenye hoteli moja mjini Udine kama ilivyozoeleka kuwa huwa wa kwanza kitendo kilichowashtua wachezaji wenzake na kushuku lazima kuna tatizo.

Katika kuhakikisha kila kitu kipo sawa mmoja ya maofisa wa kikosi cha Fiorentina alikwenda kwenye chumba cha mchezaji huyo kumuangalia na kwa bahati mbaya alikuta tayari ameshafariki dunia .

Marehemu Davide Astori ameacha mjane ajulikanaye kama Francesca pamoja na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka  miwili.

ENOCK BWIGANE

MACHI 05, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment