Responsive image
Responsive image
Posted : March 05, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Mshambuliaji wa FC Barcelona, Leonil Messi
Responsive image

Mshambuliaji wa FC Barcelona Lionel Messi ameendeleza ubabe wa kufunga mabao ya mipira ya adhabu yaani free kiki baada ya kuisaidia FC Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid.

Messi alifunga bao hilo katika dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo huo umalize dakika 45 za mwanzo huku matokeo yakiwa ni bao 1-0 lililodumu kwa dakika zote 90.

Kwa matokeo hayo Barcelona imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa la ligi kwa kufikisha alama 69 ikiwa ni alama 8 tofauti na Atletico Madrid waliopo kwenye nafasi ya pili  na alama 61.

Bao la Messi dhidi ya Atletico Madrid linamfanya kuweka rekodi ya kufunga bao la 600 akiwa na FC Barcelona.

Katika matokeo mengine ya michezo ya La Liga hapo jana Levante wakiwa nyumbani wametoka sare ya bao moja kwa moja na espanyol, real sociedad wamechomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya alaves wakati valencia wakiinyuka real betis mabao mawili kwa bila.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment