Responsive image
Responsive image
Posted : March 04, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Jengo la Ikulu ya Marekani
Responsive image

Mwanamume mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani Mjini Washington.

Kwa mujibu wa kikosi cha ulinzi wa rais mwanamume huyo alikaribia ukuta unaozunguka Ikulu katika barabara ya Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa.

Polisi wamesema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo ambapo pia jina la mtu huyo bado halijatangazwa.

Kumekuwa na matukio kadha yanayotishia usalama katika eneo la Ikulu ya Marekani ambapo mwezi uliopita mwanamke mmoja alikamatwa kwa kuendesha gari kuelekea kwenye kizuizi cha Ikulu.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment