Responsive image
Responsive image
Posted : March 03, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Maelfu ya watu nchini Slovakia wakiandamana kulaani mauaji ya mwandishi wa habari
Responsive image

Maelfu ya wananchi wa Slovakia wameandamana katika maeneo mbalimbali nchini humo ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha mwandishi mmoja wa habari na mchumba wake waliouawa kwa kupigwa risasi wiki iliyopita.

Jan Kuciak ambae alikuwa mwandishi wa makala kuhusu rushwa na mchumba wake Martina Kusnirova walipigwa risasi nyumbani kwao mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Bratislava.

Waandamanaji hao katika miji 25 walikua wakishinikiza serikali ya nchi hiyo kutovamia waandishi wa habari ambapo watu 7 wamekamatwa na polisi wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Kuciak mwenye umri wa miaka 27 aliuliwa kabla ya kukamilisha makala yake ya rushwa inayoendeshwa na wafanyabiashara wa Italia ambapo hata hivyo makala hiyo ilichapishwa baada ya kifo chake.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment