Responsive image
Responsive image
Posted : March 02, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Moshi mweusi ukifuka katika mashambulizi huko Ouagadougou, Burkinafaso
Responsive image

Milio ya risasi na milipuko imesikika karibu na makao makuu ya jeshi na ofisi za ubalozi wa ufaransa katika mji mkuu wa Burkinafaso,Ouagadougou.

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema watu waliokuwa na silaha walishuka kwenye gari na kisha kuanza kuwashambulia kwa risasi huku wakielekea ndani ya ofisi za ubalozi wa Ufaransa.

Picha za video zimeonyesha moshi mweusi ukifuka ambapo polisi wamesema wamechukua tahadhari kufuatia tukio hilo.

Washambuliaji wanne wameuawa na polisi katika eneo la ubalozi wa Ufaransa na wengine wawili wameuawa karibu na jengo la makao makuu ya jeshi.

Habari zaidi zinasema kuwa baadhi ya polisi wameuawa katika shambulio hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment