Responsive image
Responsive image
Posted : March 02, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya wachezaji wa Simba walipokuwa wakishangilia moja ya bao walilofunga katika mchezo wao dhidi ya Stand United
Responsive image

Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba wamepunguzwa kasi na Stand United chama la wana baada ya kulazimishwa sare ya mabao matatu kwa matatu katika mchezo wa mzunguko wa 20 uliopigwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es salaam.

Simba walitangulia kuziona nyavu za Stand United kwa mabao mawili ya mapema yaliyofungwa na mlinzi Asante Kwasi katika dakika ya sita na Nicolas Gyan katika dakika ya 23 kabla ya chama la wana kusawazisha mabao hayo katika dakika za 35 na 41 matokeo yaliyodumu hadi dakika 45 za awali zilipomalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu ambapo Simba kama kawaida walipata bao la TATU katika dakika ya 61 likifungwa na Nicolas Gyan kabla ya Stand kusawazisha katika dakika ya 66 kupitria kwa Bigirimana Blaise matokeo yaliyodumu hadi dakika tisini.

Kwa matokeo hayo Simba wanaendelea kusalia kileleni kwa kufikisha alama 46 ikiwa ni alama 6 tofauti na mahasimu wao Yanga waliopo kwenye nafasi ya pili na alama 45 huku simba wakiwa tayari wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Yanga na Stand United wenyewe wamepanda hadi nafasi ya nane kwa kufikisha alama 21.

OSCAR URASSA

MARCHI 02, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment