Responsive image
Responsive image
Posted : March 01, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyerwa Daniel Damian
Responsive image

Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kyerwa mkoani Kagera wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani wakiwemo wenyeviti wa vitongoji na wanachama wengine  17.

Wakikabidhi kadi kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyerwa  Daniel Damiani, madiwani hao    wamesema sababu iliyowafanya kuhamia CCM ni kuridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.

Tulakila Twijuke aliyekuwa diwani wa kata ya Bugomora  na Sadath Jeremiah aliyekuwa diwani wa kata ya Kibare walilakiwa na viongozi wa CCM baada ya kujiunga na chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Bugomora

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kyerwa Daniel Damian amepongeza uamuzi huo na kuwataka  viongozi wa CCM ngazi za kata na wilaya kuendelea na kazi ya  kutatua kero za wananchi.

Naye Katibu wa siasa itikadi na uenezi CCM mkoa wa Kagera Hamim Mohmoud amepinga uvumi ulioenea kuwa CCM inafanya hila kununua viongozi wa vyama vya ushindani.

CHARLES MWEBEYA

28 FEBRUARI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment