Responsive image
Responsive image
Posted : February 27, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Responsive image

Serikali inatarajia kuajiri walimu elfu kumi na nne  wa shule za msingi na sekondari  wakiwemo walimu walioko vyuoni ili kupunguza changamoto ya upungufu wa waalimu katika shule hizo.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kasim  Majaliwa  alipokuwa katika chuo cha ualimu cha Kitangali Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara ambapo amesema serikali inataka kuleta ufanisi wa kazi kwa waalimu katika kutekeleza majukumu yao.

Akizungumza na wanachuo Waziri Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali imetenga nafasi elfu kumi na nne  za ajira ya walimu   wa shule za msingi na sekondari ili kutatua adha  ya upungufu wa walimu.

Akiwa katika msafara wake Waziri Waziri Mkuu Majaliwa amezungumza na wananchi wa vijiji vya Chungutwa na Kitangali  waliolalamikia kero ya maji, na umeme ambapo amesema serikali inaendelea kutenga fedha za kuboresha miundombinu yake ili kutatua kero hizo  kwa wakazi waishio vijijini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo amesema serikali imetenga fedha kwa ajili ya kukarabati vyuo vinne nchini ili kuongeza udahili.

TATU ABDALLAH

27 FEBRUARI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment