Responsive image
Responsive image
Posted : February 24, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
Responsive image

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametoa wito kwa madiwani wa Halmashauri ya mji wa Kahama na Msalala mkoani Shinyanga kuwasimamia watendaji wa sekta ya ardhi ili kuongeza kasi ya upimaji wa maeneo katika wilaya hiyo.

Akizungumza mkoani humo katika mkutano maalum uliowashirikisha madiwani wa halmashauri hizo, Waziri Lukuvi amesema asilimia 90 ya makazi katika mji wa Kahama hayajapimwa hali inayosababisha wananchi wengi kutonufaika na makazi wanayoyajenga.

Akizungumzia  mfumo wa kukusanya kodi ya ardhi Waziri huyo ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama kuhakikisha wenye hati za kimila hawatozwi kodi.

GREYSON KAKURU

FEBRUARI 24, 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment