Responsive image
Responsive image
Posted : February 23, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli (katikati) na Rais Uhuru Kenyata wa Kenya (kulia kwake) wakiwa Uganda kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
Responsive image

Rais  Dkt. John Magufuli na  Rais Uhuru Kenyata wa Kenya wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kutatua tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza katika biashara kati ya nchi hizo mbili.

Marais hao wametoa maagizo hayo leo  walipokutana na kufanya mazungumzo  mjini Kampala muda mfupi kabla ya kuanza kwa vikao vya mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika mazungumzo yao, Marais hao  wamesema wanataka kuona biashara kati ya Tanzania na Kenya inazidi kukua na bidhaa zinauzwa na kununuliwa baina ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote na  kuagiza tofauti zilizojitokeza katika baadhi ya bidhaa zimalizwe.

Viongozi hao wametoa  maagizo hayo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma na Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kaskazini wa Kenya Mhe. Peter Munya.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment