Responsive image
Responsive image
Posted : February 23, 2018 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa nchini Uganda
Responsive image

Mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika leo mjini Kampala, Uganda ambapo Tanzania imewakilishwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Hapo jana wakuu wa Jumuiya hiyo wamekutana kujadili maendeleo na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya sekta ya miundombinu na afya ambapo Rais John Magufuli ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusimamia vizuri rasilimali walizonazo ili kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu na kuimarisha huduma za afya.

Imeelezwa kuwa katika miaka 10 ijayo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitahitaji Dola za Marekani Bilioni 78 kutekeleza miradi ya miundombinu inayopendekezwa.

Akizungumza katika mkutano huo Rais Dkt. John Magufuli amesema pamoja na kutumia mfumo wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ( PPP) ni muhimu serikali za kila nchi kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya kodi na rasilimali nyingine ili kutekeleza miradi ya miundombinu, afya na sekta nyingine.

Rais Magufuli ametolea mfano wa miradi iliyoanza kutekelezwa hapa nchini ukiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) na ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge) kuwa serikali ya Tanzania imeanza kutekeleza miradi hiyo kwa kutumia fedha zake baada ya kufanikiwa kusimamia vizuri rasilimali zake.

Marais waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Silva Kiir wa Sudan Kusini huku marais wa Rwanda na Burundi wakiwakilishwa.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment