Responsive image
Responsive image
Posted : February 22, 2018 (4 weeks ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Marekani Donald Trump
Responsive image

Rais wa Marekani Donald Trump amesema walimu wenye silaha wangeweza kuzuia mauaji yaliyotokea shuleni wiki iliyopita na kusababisha vifo vya wanafunzi kumi na saba katika mji wa Florida.

Rais Trump ametoa mapendekezo hayo kwa manusura wa mauaji ya Februari 14 na kusema wanahakikisha tukio kama hilo halitokei tena.

Pendekezo la Rais Trump limekuwa likiungwa mkono kwa muda mrefu na Shirikisho la Silaha la Marekani (NRA) kundi lenye ushawishi mkubwa wa matumizi ya bunduki nchini humo.

Rais huyo kutoka chama cha Republic pia ameunga mkono wito wa kuwachunguza watu wanaonunua silaha huku akionekana kutounga mkono hoja za kutaka mabadiliko ya sheria ili kuthibiti umiliki wa silaha nchini humo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment